Monday, January 15, 2007

Ech ya Abiria.

Juzi nilikuwa naenda mtaani,na nilipanda basi la 2M,58.Kulikuwa na joto sana,ile joto ya kutabiri mvua.Mama mmoja akaingia kukaa karibu na mimi,upande wa dirisha.Akawa ajipepetapepeta kwa kijikaratasi huku ameliinua shati lake kidogo kifuaniNikamuuliza mbona asifungue dirisha-akajariiiibu,ikakwamwa.Alikuwa hana starehe hata.
Nikamhurumia nikamwambia wacha basi tufungue hiyo iko mbele kidogo.Nafikiri alishindwa mbona huyu naye kanishugulikia hivi.Mara ndiye huyu yuanza kucheka.Nikamuuliza-wafurahia nini,niambie nami nicheke pia-
Akasema-shukuru Mungu wewe bado kijana.Si ati kuna joto jingi vile,ni ech{age}.
Ukifika umri kama wangu hata wakati wa baridi jasho latiririka kama maji.Mtu hujiskia kama waweza tembea uchi.Unaona?!-Akaendelea huku acheka na jujipangusa jasho shingoni akitumia kitambaa kikubwa.
-Hii joto yaweza kukufanya ukafungilia taulo shingoni-Akasema.
Nilijihisi kuangua kicheko.Lakini nilijikaza na kutabasamu kistaarabu.

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home