Monday, April 02, 2007

Siku Saba

Kila wakati nafikiria nalisema jina lako
Nalia.
Uso wako wa huzuni hauondoki
Akilini
Naumia.
Niliwashwa kukuona vile.
Maisha yangu kayagawa katikati.
Naamini upendo.
Naamini ukweli pia.
Upendo ni mvuto wa nguvu.
Sababu nakupenda, nilikupenda
Siku ya kwanza ulipoongea.
Mivuto hii, maisha haya.
Ndani ya ukweli nakosea hisia zangu.
Hisia zangu za ukweli kwamba nakupenda.
Nataka kukupenda……
Lakini,
Maisha niliyoyachagua
Yaniondoa
Nakuweka mbali
Nikiwa nachomwa Ndani,
Sababu ya kukupenda,
Sababu hufai kujua haya……
Kheri ungejaribu kuelewa,
Najua wajaribu, wakati mwingine kupenda,
Kujua,
Kupotewa.
Nataka kukupenda!

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home